This archive report was first published on 10 July 2019.
Rais Uhuru Kenyatta akiwa na Gavana wa Mombasa Hassan Joho (katikati) na Mwenyekiti wa Uchumi wa baharini Jenerali Samson Mwathethe (kushoto) wakizuru idara ya uhandisi katika uzinduzi wa Bandari Maritime Academy.
Wabunge waliokuwepo kwenye uzinduzi huo walionekana kana kuwa hawajajitayarisha kikamilifu, huku wakiongozwa na Abdulswamad Nassir wa Mvita.
Wabunge hawa walikuwa wamejikuta kwenye njia panda iwapo wabunge watafika kutokana na msimamo wao mkali au wataukwepa mkutano huo wa rais.
Wakati wa kuwasikiza maunyeunye yao, Gavana Hassan Joho alihusishwa mapema juu ya sherehe za uzinduzi kupitia kwa mwenyekiti wa uchumi samawati Samson Mwathethe na Rais Uhuru Kenyatta.
Wadadisi wa masuala ya mwambao wanasema kuwa kuwepo kwa Gavana Joho kulisaidia kupunguza lawama na aibu kwa wabunge waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa chuo cha Bandari Maritime Academy.
Wabunge waliokuwepo walionekana wanyonge kwa fedheha za kupinga mswada unaohusiana na huduma za shirika la shehena za bandarini nchini la Kenya National Shipping Line (KNSL) bungeni.
Waliopata fursa ya kukaa jukwaani la rais pamoja na magavana watatu wanaokurubana na ufuo wa bahari hindi moja kwa moja, Hassan Joho (Mombasa), Salim Mvurya (Kwale) na Fahim Twaha (Lamu), walionekana kana kwamba wamekalia viti vyenye misumari ama miba wakibabaika kwamba huenda msemaji mmoja hadi mwingine anayetoa hutuba anaweza kuwakejeli.