Maseneta kuendesha vikao vya kukusanya maoni kuhusu mswada wa mageuzi ya sheria za vyama

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 11 January 2022.

Seneti inaendesha vikao vya kukusanya maoni kuhusu mswada wa mageuzi ya sheria za vyama

Seneti imeanza kukusanya maoni na mapendekezo kutoka kwa umma kuhusu mswada wa mageuzi ya sheria za vyama vya kisiasa. Mswada huo ulipitishwa rasmi katika Seneti mwezi Januari 2022.

Shughuli hiyo ya kukusanya kauli za umma kwa njia ya taarifa na mawasilisho ya moja kwa moja, itaendeshwa na Kamati ya Seneti kuhusu Haki, Masuala ya Kikatiba na Haki za Kibinadamu.

Kamati hiyo inayoongozwa na Seneta wa Nyamira, Okong'o Omogeni, ina maseneta ambao ni wataalamu katika masuala ya sheria. Miongoni mwao ni; kiongozi wa wachache James Orengo, Mkuu wa Sheria wa zamani Amos Wako (Busia) na kiranja wa wachache Mutula Kilonzo Junior.

“Naamuru kwamba mswada huo uwasilishwe kwa kamati ya seneti kuhusu sheria ili iweze kuendesha vikao vya kukusanya maoni na mapendekezo kutoka kwa umma,” akasema Bw Lusaka.

Seneta wa Pokot Magharibi, Samuel Poghisio, alihakikisha kwamba mjadala kuhusu mswada huo utaendeshwa bila vurumai zozote. “Sarakasi tulizoshuhudia katika bunge lile lingine, zilishusha hadhi ya asasi ya bunge. Lakini tunaweza kurejesha heshima na hadhi hiyo,” akasema Bw Poghisio.

Januari 25, 2022, itakuwa siku ya mwisho ya kukusanya maoni na mapendekezo kutoka kwa umma. Baada ya hapo, kamati ya Bw Omogeni itaandaa ripoti na kuwasilisha ripoti yake kwa kikao cha bunge lote.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...