Wakenya Wachangamka Kuhusu Shule ya China Kuanza Kufunza Lugha ya Kikuyu

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 9 July 2019.

Shule moja ya China imeanza kufunza lugha ya Kikuyu kwa wanafunzi wake, kati ya zile zinazofunzwa katika shule za Kenya.

Hisia kali zimekuwa zikiendelea nchini humu kuhusu nafasi ya Wachina, hasa baada ya serikali ya Rais Uhuru Kenyatta kuingia mamlaka.

Wakati wa kuchukua mikopo na kupeana zabuni za kazi, serikali ya Jubilee imekuwa ikichukua kampuni za China kwa ajili ya ujenzi wa barabara humu nchini.

Wiki kadhaa zilizopita, mjadala ulikuwa umeibuka baada ya habari kuibuka kuwa kuna Wachina wanaojiingiza katika biashara ndogo ndogo humu nchini, kama vile kuchoma mahindi mitaani na kuuza nguo za mitumba katika soko kuu la Gikomba jijini Nairobi.

Video moja iliyopakuliwa mtandaoni na msanii Daniel Ndambuki, Churchill, inazidi kusambaa huku Wakenya zaidi wakitoa maoni yao kuhusu hatua hiyo.

Wanafunzi katika shule hiyo ya China wanafunzwa lugha ya Kikuyu, ambayo ni moja wapo wa lugha za mama katika jamii za Mlima Kenya, ikiwemo familia ya Rais Uhuru Kenyatta.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...