This archive report was first published on 8 July 2019.
Shughuli za mazishi za Mohammad Furqan, kutoka mtaa wa Uttar Pradesh, ziliishia kwa kushuhudia kizazaa baada ya jamaa kufufuka wakati wa mazishi yake mnamo Juni 21, 2019.
Alipomalizwa katika hospitali moja, Furqan alitangazwa kufariki, lakini familia yake ilijulishwa kuwa jamaa wao alikuwa 'amefariki' kwa sababu hawakuwa na fedha za kugharamia malipo.
Alipelekwa nyumbani na shughuli za mazishi zikaanza, lakini 'maiti' alionekana akiamka na kuzua kizazaa huku waombolezaji wakiwa mguu niponye kila mmoja.
Alisema, "Tulikuwa tunaendelea na shughuli za mazishi wakati ambapo tuliona maiti akiamka. Alikimbizwa katika hospitali ya Ram Manohar Lohia na madaktari wakasema hakuwa amefariki."
Madaktari wanasema Furqan yuko katika hali mahututi lakini yungali hai, na daktari mkuu wa Lucknow Narendra Agarwal alidhibitisha tukio hilo na kusema litachunguzwa zaidi.