Skip to main content

Philomena Mwilu: Maisha Yangu Yamo Hatarini

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 7 July 2019.

Naibu jaji mkuu Philomena Mwilu anahofia maisha yake huku akidai kuna njama ya kumwangamiza tangu mahakama ya upeo ilipobatilisha uchaguzi wa urais mwaka wa 2017.

Alisema amekuwa akifuatwa kimya kimya na magari kadhaa pamoja na kupigiwa simu na watu asiowajua.

Naibu jaji mkuu Philomena Mwilu. Mwilu amesema maisha yake yamo hatarini. Picha: Nation

Aliongea na gazeti la Standard, jaji huyo alisema amekuwa akiishi kwa woga mwingi lakini ameamua hatajiondoa katika wadhifa wake kama naibu jaji mkuu.

"Nimekuwa nikifanya kazi yangu kwa uadilifu, na kama nilivyoahidi kuilinda katiba ya Kenya kama mojawapo wa majaji wakuu nchini. Hata wakiniua kama vile wamekuwa wakijaribu kufanya, nitaendelea kufanya kazi yangu kama jaji bila woga," Aliambia gazeti hilo.

Alisema kwa sasa hata kwenda kanisani ni tatizo kwani anahofia kuna genge linamfuata kung'oa uhai wake.

"Sijawahi kuwa na wasiwasi hivi maishani mwangu. Lakini hakuna ninalofanya ila tu kumwamini Mwenyezi Mungu," Alisema Mwilu.

Alikuwa miongoni mwa majaji waliobatilisha uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 8 2017. Picha: Standard

Alisema maisha yake yalichukua mkondo mpya huku akiamini kuna kundi ambalo limekuwa likimpangia mabaya.

Alisema hata kiongozi wa mashtaka ya umma Noordin Haji na mkuu wa DCI George Kinoti walikuwa wamemfungulia Mwilu mashtaka akidaiwa alihusika na kosa la utumizi mbaya wa afisi yake alipofanya biashara zake na benki moja humu nchini.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →