Msanii wa nyimbo za kikazi kipya, Enock Wilson Teyie maarufu Rusty Gee, amekuwa akipigana na matumizi ya mihadarati pia visa vya ubakaji kupitia muziki tangu mwaka 2015.
Mapema mwaka huu, serikali ya Kaunti ya Vihiga kupitia wizara ya vijana na michezo ilianzisha tamasha la sanaa kwa jina Vihiga Extravanza, ambalo lilikuwa na lengo la kutambua wasanii wanaokuja eneo hilo.
Msanii huyu alisema kuwa serikali iligharamia ada ya kurekodi nyimbo tatu kwa wasanii hao, na kuonyesha furaha kwake kwamba kupitia jitihada zake serikali hiyo imeanza kukumbatia sekta ya burudani eneo hilo.
Msanii huyu anashukuru Waziri wa wizara hiyo, Felistus Okumu na kamati yake nzima kwa kukubali kuandaa tamasha hiyo.
Msanii huyu (Rusty Gee) anajivunia kuachia teke kadhaa zinazozidi kutesa anga ya muziki wa burudani, ambapo sasa anatamba na kibao cha Sugarmummy.
Msanii huyu anasema anavutiwa na teke za injili kama ‘Hela,’ Utawala,’ – kazi yale, wimbaji na mtunzi wa hapa nchini maarufu kama Juliani.
Msanii huyu anashauri wasanii chipukizi wanaolenga kufanya vizuri kwamba mwanzo wanastahili kuonyesha ni dhamu na kuelewa wanacholenga katika taaluma hii fana bila kuweka katika kaburi la sahau kuwa kukumbana na pandashuka ni jambo la kawaida.