Mshukiwa wa Wizi wa Kimabavu Anaswa Mtaani Umoja

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 2 July 2019.

Mshukiwa wa Wizi wa Kimabavu Anaswa Mtaani Umoja

Julai 1, 2019 - Mtaani Umoja, Nairobi

Mshukiwa wa wizi wa kimabavu alikamatwa mtaani Umoja, Nairobi, akiendesha gari la wizi ambalo lilikuwa limeibwa kutoka kwa afisa mkuu wa serikali.

Gari hilo, linalojulikana kama Toyota Prado VX, lilikuwa limeibwa kutoka kwa makaazi ya Balozi Jean Wambui Kimani mtaani Kileleshwa takriban saa ishirini zilizopita.

Maafisa wa DCI walimfumani mshukiwa, Calvin Amangune Amata, akiendesha gari hilo la wizi wakati akijaribu kukwepa mtego wa polisi.

Stakabadhi za benki, za biashara na bidhaa nyinginezo za kibinafsi zilipatikana katika kipochi cha mshukiwa.

Wakati maafisa hao wakimkagua mshukiwa, walipata stakabadhi kadhaa za benki, za biashara na bidhaa nyinginezo za kibinafsi.

Uchunguzi unaendelea na tunatarajia kuwakamata washukiwa wengine ambao wangali mafichoni.

Washukiwa hao walitoweka na gari hilo lenye thamani ya KSh 8 milioni, televisheni yenye thamani ya KSh 40,000, mikufu yenye thamani ya KSh 300,000 na simu zake tatu za rununu (iPhone, Tecno na Samsung).

Source: Tuko

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...